Isaac Lamoka

4359

Isaac Lemoka ni mmoja wa watangazaji kinara wa habari katika runinga ya KBC. Ni mtangazaji wa Darubini ya Channel 1 saa moja usiku, na vile vile Dunia wiki Hii Jumamosi saa saba unusu mchana.

KBC Radio_KICD Timetable

Amehusika katika kufahamisha wakenya na dunia kwa ujumla kuhusu matokeo ya muhimu kuwahi kufanyika katika historia ya Kenya.

Mwaka 2013 aliripoti moja kwa moja jinamizi la West Gate jijini Nairobi lililotekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab ambapo watu Zaidi ya 70 walipoteza maisha yao na mamia kujeruhiwa.

Ameripoti moja kwa moja Uchaguzi mkuu wa 2013 nchini Kenya, na kadhalika chaguzi za vyama vya kisiasa.

Get breaking news on your Mobile as-it-happens. SMS ‘NEWS’ to 20153

Kando na televisheni Lemoka aidha ni mtangaziji wa Radio Taifa, moja wapo wa radio za shirika la Utangaziji nchini Kenya KBC. Anahusika pakubwa na matangazo ya moja kwa moja ya soka na kurindima katika matangazo ya siku kuu za kitaifa.

 Lemoka alijiunga na shirika la KBC mwaka wa 2012 baada ya kuhitimu na stashahada ya Uanahabari kutoka katika taasisi ya MultiMedia na hivi sasa anasomea shahada ya maswala ya nchi za kigeni na usalama katika Chuo kikuu cha Nairobi.

Lemoka ni mcheshi mwenye makeke na mbwembwe kazini.

Anajipa raha kwa kutazama soka, kuogelea na safari za mbali kila apatapo fursa

Katika mitandano ya kijami utasema naye kupitia TwitterFacebook na Instagram

KBC-You-tube-728x90-New-2

Tell Us What You Think


SHARE