Mtaala mpya wa elimu wa CBC uliasisiwa nchini Kenya mwaka wa 2017 baada ya mfumo wa 8-4-4 kutumika humu nchini kwa takriban miaka 35 tangia mwaka wa 1985 ulipoanzishwa na aliyekuwa rais wa pili wa Kenya hayati Daniel Toroitich arap Moi.
CBC ni mfumo unaoegemea zaidi upande wanafunzi na unaozingatia zaidi uwezo wa mwanafunzi wa kujifunza mwenyewe na kukuza ujuzi unaohitajika siku za usoni katika ustawi wa kiteknolojia itakayofaa nchi yetu katika kutatua matatizo mbalimbali katika karne hii ambapo teknolojia inaonekana kukumbatiwa kote ulimwenguni.Kaunti ya Mombasa ndio kaunti ya kwanza nchini Kenya kukumbatia mafunzo ya robotics kwa wanafunzi wa kati ya miaka mitatu hadi sita walioko chini ya mtaala wa CBC kama anavyonieleza mkuu wa idara ya teknolojia ,habari na mawasiliano Anwar Ahmed katika kaunti ya Mombasa.
By Clavery Khonde