Pwani FM

Pwani FM: Elungata asema huduma za Feri zitaondolewa endapo maambukizi ya Covid 19 yataongezeka Mombasa

Mshirikishi wa Pwani John Elungata ameleeza kuwa kuongezeka kwa maambukizi ya homa ya Corona katika Kaunti ya Pwani ni kutokana na upimaji watu kwa wingi (mass testing) ambayo serikali imeanza kufanya.

Akizungumza na  mwanahabari Dalila Athman leo asubui Elungata amesema tangu zoezi la kupima wafanyikazi wa bandari ya Mombasa, kufikia jana kulikua na watu wapatao 12 walioambukizwa virusi vya Corona na huendi zoezi hilo katika bandari likakamilika katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Elungata aidha ameeleza kuwa wataanza mchakato wa kupima watu homa ya Corona katika kivuko cha ferry, na iwapo kutapatikana na visa vya maambukizi serikali itasitisha huduma za ferry katika kivuko hicho, kwa sababu baadhi ya wafanyikazi wa Bandari (KPA)  pia wanaishi Likoni.


Kuhusu kuondolewa kwa kafyu, Elungata ameeleza kuwa itategemea jinsi watu watakavotii vile wanavyoagizwa na serikali kufanya. Amesema iwapo maambukizi yataenea basi serikali haitaweza kuondoa sheria hiyo.

Related posts

The MashavTop10

Eric Munene

MASAUTI:Kuna watu wanajaribu kujenga chuki mimi na Joho tuko poa

Ken Wekesa

Pwani Jioni : Badi Twalib asifia uongozi wa ODM

Eric Munene

Leave a Comment