Pwani FM

Diamond atimiza ahadi kwa familia 57

Diamond platinumz ametoa msaada kwa familia 57 kati ya familia 500 ambazo alikuwa ameahidi kuzilipia kodi kwa muda wa miezi mitatu.

Aidha Diamond amempa nafasi mamake Bi Sandra Kassim kusaidia kutekeleza jukumu hilo mitaani ambapo amesema kuwa wanapania kusaidia familia zenye watu walemavu, wajane na watu wanaokabiliwa na magojwa sugu.

Diamond pia amekuwa akiwatembelea wagonjwa katika mitaa mbali mabali mjini Dar er salam na kutoa msaada kwao.

Mapema wiki iliopita Diamond alitangaza kuwa atazilipia kodi ya miezi mitatu familia 500 wakati huu wa janga la covid 19.

Related posts

Pwani FM: Wazee wa Kaya wamtaka Gavana Kingi kuishauri serikali kuu kutumia mitishamba kukabiliana na Korona

Eric Munene

Hivi nasubiria Rais atasema nini..

Eric Munene

Pwani FM: Balozi wa Marekani Asema Milioni 705 Walizozipa Kenya ni Lazima Zitumeke Kukabili Covid 19

Ken Wekesa

Leave a Comment