Pwani FM Uncategorized

Serikali yaanza harakati za kuwafidia waathiriwa wa bwawa la Mwache katika eneo bunge la Kinango.

Akizungumza  kwenye jukwa la  Uchambuzi na Swala Nyeti, meneja wa idara ya utafit na mipango ya miradi ya mamlaka ya maendeleo ya Pwani (CDA) Mwasiti Bendera  amesema kuwa kwa sasa mipango ya kuwaondoa wakaazi ambao wapo katika sehemu iliyotengewa ujenzi wa bwawa hilo imeanza.

Ameelezea kwamba mamlaka hiyo ikishirikiana na tume ya ardhi na wizara ya maji inahakikisha kuwa watakaoathirika wanaondoka kwa amani  kwa kupewa fidia.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa mamlaka hayo  Mohammed Keinan amesema ujenzi wa bwawa hilo utanufaisha wakaazi wengi wa kaunti za Kwale na Mombasa huku akisema kuwa mradi huo utazidisha juhudi za unyunyuziaji na uzalishaji wa chakula

Related posts

chomeka

Eric Munene

Mwanasaikolojia Collins Bollo asema ni jukumu la mwanafunzi kujilinda.

Eric Munene

Mchakato wa kuunda chama cha Pwani kumekuwa na gumzo kwenye vyombo vya habari

Eric Munene

Leave a Comment