Pwani FM

Vijana Kilifi Wapata Mafunzo ya Kuzuia Mimba za Mapema.

Serikali ya kaunti ya Kilifi kwa ushirikiano na shirika la DSW linaendelea kuwapa vijana  mafunzo ya mbinu za  maisha maarufu kama life skills za kudhibiti mimba za mapema na kuwasaidia wasichana waliopata mimba za mapema  mbinu za kuishi na kujikimu kimaisha.

Joyce Muteki ni mwanafunzi wa darasa la tano katika  shule ya msingi ya Shangia huko Kaloleni  katika kaunti ya Kilifi.

Japo ana umri mdogo ni mkufunzi wa mbinu za maisha. Alidhaminiwa  mafunzo hayo na shirika la DSW linaloendesha miradi mbali mbali ya kuwasaidia vijana katika kaunti ndogo ya Kaloleni.

Na mara kwa mara amekuwa na ujasiiri wa kuwahamasisha wenzake ili kuwashawishi wasishiriki ngona na kusababisha mimba za mapema.

Kenneth Miriti ni mshirikishi wa afya ya uzazi ya vijana, watoto na kina mama katika kaunti ya Kilifi.

Anasema kwamba Joyce na wenzake wengine wamekuwa msaada kuwahamasisha wanafunzi wenzao walioko katika shule za msingi kuhusiana na hatari na kuepuka mimba za mapema.

Ameambia Pwani FM kwamba kupitia juhudi za shirika hili la DWS na mashirika mengine, visa vya mimba za mapema vimepunguwa kwa kiwango kikubwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka uliopita.

Pia anaelezea kwamba  wasichana walioathirika wanapewa mbinu hizi za maisha ili waweze kujikimu kimaisha.

Mshirikishi huyo amefichua kwamba pia kuna makundi ya vijana yanayowahamishisha wenzao kuhusiana na mafunzo ya afya uzazi katika kaunti nzima ya Kilifi kama njia nyingine ya kudhibiti visa vya mimba za mapema.

Zaidi ya wahudumu wa afya 200 katika kaunti hiyo pia wamepewa mafunzo ya mbinu za maisha na huwapatia vijana wanaotembelea vituo tofouti vya afya.

 

 

 

Related posts

Pwani Mchana: Hatimaye naibu wa rais Dkt. William Ruto amesema mipango inafanywa

Eric Munene

Pwani FM: Gavana wa kaunti ya Kilifi amepinga vikali kuhusiana na vifo vya watoto 17

Eric Munene

PWANI FM: Joho asema tabia ya watu wetu kutangamana na kupuuza Social distancing ndio inaendeleza maambukizi ya COVID 19.

Ken Wekesa

Leave a Comment