Newest Episode Pwani FM

Vuguvugu la fast action linapania kuwatimua mamlakani wabunge wasaliti

Vuguvugu la fast action linalopania kuwatimua mamlakani mbunge wa Kisauni Ali Mbogo na mwenzake wa Likoni Mishi Mboko wamesema viongozi hao wamechangia kwa kulemaa kwa uchumi eneo la Pwani baada ya kukataa kuunga mkono hoja ya Mbunge wa Nyali Mohamed Ali ya kutaka kuondolewa afisini waziri wa uchukuzi James Macharia.
Wakizungumza katika kipindi uchambuzi n swala nyeti mwenyekiti wa vuguvugu hilo Salim Karama na katibu mwandamizi Hariet Muganda, wameeleza wameanza na mchakato wa kuwabanduwa wawili hao ili iwe funzo.
Wamesema vijana wengi wamekosa ajira na kampuni kufungwa kutokana na agizo la waziri Macharia.
Aidha vuguvugu hilo limekanusha madai kuwa linafadhiliwa na wanasiasa ili kuwachafulia majina Mbogo na Mishi, na kueleza kuwa vuguvugu hilo si la kisiasa na wala halina mafungamano na kundi wala chama chochote cha kisasa.

Related posts

Radio Taifa: Siku ya Kifua kikuu Duniani

English Service Podcaster

Real men like Pday do this always

Eric Munene

Kundi la wawakilishi wadi kutoka kaunti ya Mombasa limeibua madai ya kufujwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 31

Eric Munene

Leave a Comment