Newest Episode Radio Taifa

Yaliyotukia: Serikali yazindua #KaziMtaani

Serikali imezindua mpango wa kitaifa wa kutoa huduma za usafi katika mitaa ya mabanda nchini al maarufu kazi mtaani.

Kulingana na Katibu Katika Idara ya Nyumba Patrick Bucha tayari zaidi ya watu 26,000 wameajiriwa katika awamu ya kwanza pekee kutoka kaunti nane nchini ambazo ni: Nairobi, Kwale, Mombasa, Kisumu, Nakuru, Kiambu, Kilifi na Mandera.

Bucha anasema kuwa mitaa zaidi ya mabanda kutoka kaunti hizo nane, pamoja na kaunti nyingine zitakazonakili maambukizi ya juu ya ugonjwa wa Covid 19 hususan kutoka mitaa ya mabanda zitajumulishwa katika awamu ya pili itakayoanza baadae mwezi huu.

Katibu Bucha alihojiwa na mwanahabari wa Radio Taifa Dismus Otuke.

Related posts

Mayienga FM: Weche Manyien Saa Achiel Mokinyi: 11th May 2020

English Service Podcaster

KBC English Service: Important note for Kenya’s unity

Carolyne Gachacha

KBC English Service: Kenya has a false middle class

Carolyne Gachacha

Leave a Comment