President Uhuru’s off-cuff remarks during labour day celebrations

President Uhuru Kenyatta’s off-cuff remarks during Labour Day event at State House-Nairobi. May 1, 2020.

Ningependa tu kuongezea machache. Na hayo machache ni kuendelea kuuliza Wakenya tujichunge. Tujichunge wakati huu mgumu. Na najua mimi ya kwamba kuna wengi ambao wanapitia mashida kwa sababu ya huu ugonjwa. Ugonjwa ambao hatukujiletea umetoka nje lakini uko nasi. Na lazima kama Wakenya tushirikiane, tuungane pamoja ndiyo tuhakikishe ya kwamba tumepambana na tumeshinda vita kati ya huu ugonjwa.

Huu ugonjwa hautashindwa na serikali peke yake. Na sitasita kurudia. Huu ugonjwa utashindwa tukishirikiana na tukiungana pamoja kama Wakenya. Hiyo ndiyo njia pekee. Ndiyo tuweze kurudisha uchumi wetu.

Na kwa huu muda ambao tuko na huu ugonjwa, kama Serikali tutaendelea kuona ni kwa njia gani tutasaidiana na Wakenya wenzetu haswa wale ambao wamelemewa kabisa na tuone ni kwa njia gani tutaweza kuwasaidia katika wakati huu mgumu ambao tuko nao. Na ndipo juzi kati ya mikakati ambayo nilitangaza, nilisema  ya kwamba ndiyo tuweze kusaidia haswa wafanyakazi  wale wa chini kabisa, tukaongeza idadi ya watu ambao hawatakuwa wakilipa kodi. Nimekisikia ndugu Atwoli akisema tuongeze hata zaidi, tutajaribu kulingana na uwezo, lakini pia taifa haiwezi kujengwa bila kodi. Lakini tutaendelea kuona ni kwa njia gani tutaweza kusaidia. Tumejaribu sana ndiyo tuweze kupunguza bei ya vyakula na mengineo. Tukatangaza ya kwamba tumeshukisha VAT kutoka aslimia 16 mpaka aslimia 14 (14 percent) hiyo yote tumefanya ndiyo tuweze kuona ni kwa njia tutaweza kusaidai wananchi haswa wale wadogo wa chini. Na tutaendelea, hii program ambayo tumeanza ya ‘kazi mitaani’ tunataka vijana wetu waweze kuwa wanapata riziki yao wakitusaidia kusafisha mitaa yetu, kutengeneza barabara zetu na mambo mengine kama haya.

Na mimi ningependa sana sana, kwanza kushukuru bunge letu la Kenya kwa vile tumesaidiana pamoja na kupitisha sheria mbali mbali ambazo zimetuwezesha kufanya yale ambayo tayari tumefanya na tutaendele kufanya na tutaendelea kushirikiana. Kwa sababu, vile nilisema hapo awali kushinda huu ugonjwa, kurudisha uchumi wetu, hautachukua Uhuru pekee yake ama serikali pekee yake, itachukua sisi wote. Na hivi karibuni napanga kualika  viongozi wa vyama mbali mbali, viongozi wa wafanyakazi, viongozi wa employers, na wote, washikadau wote, tuweze tukae pamoja na tuseme tukishaa maliza kupambana na huu ugonjwa, hii uchumi yetu, tutafufua namna gani na ndiyo maisha ya mwananchi wa kawaida iweze kurudi mahali ambapo tulikuwa. Na hio itatuhitaji sis wote, na ndipo naendelea kusema, tusitumie hii vita ya Corona kama ni wakati wetu wakupiga siasa duni. Unaskia huko mwingine akisema ohhh pesa ya Corona haitumiwi vizuri, ingetakiwa itumiwe namna hii jameni tusicheze na maisha ya wakenya.

Pesa yote ambayo imetumika kupapambana na hili janga, wakati ukifika, it shall be audited in broad day light. Kila shilingi, kila ndururu ambayo imetumika wakenya waweze kujua hii pesa ilitumika kwa njia gani na kusaidia nani. We shall make it public. Hakuna kitu ambayo itafichwa. Lakini hii sio wakati wa kugombanisha, huu ni wakati ya kuokoa maish jameni, tafadhali.

Viongozi, if you have mercy on your people, this is the time for you to be supportive of the support that we are all undertaking to ensure that we defeat this virus.

Niseme pia, lazima tuangalie mbele tujue ya kwamba Corona haitakuwa na sisi maisha bado tunataka soko zetu zirudi. Jameni nilicheka juzi nikaona wengine wako hapo wanasema Uhuru anafanya makosa, anatuma maua kwa wazungu. Jameni wajua hayo maua ambayo tumetuma, Corona itaisha, hayo maua yaandika wafanyikazi maelfu na maelfu ya wakenya and they say, watu wanakumbukwa wakati wa shida. Tukiwa tumewatuma huko na wanaona hii imetoka Kenya, wajati soko itafunguliwa mtu akienda kununua maua, kitu cha kwanza atafikiria ule alinikumbuka wakati wa shida, huko ndio mimi naenda kununa maua yangu. Think before you start talking nonsense on social media.

We must protect our economy. We must look into the future; we must look at what we are going to do when we survive. This is not the time for us to be petty. This is not the time for us as Kenyans to be cheap. This is the time for us to come together. This is the time for us to work together. This is the time to plan the future of this great land.

Kwa hayo machache na mengi, nasema Mungu awabariki, Mungu awalinde, tukae manyumbani najua ni ngumu kwa wengi lakini hii ni nafasi yetu ya kujuana tena na wake zetu na watoto wetu tukiwa manyumbani . Let us not always look at the negative. Kuna opportunity ya kujuana sasa tena, na ni mema mengi inaeza kutokana na kujuana zaidi.

Kwa hivyo, mimi nasema Mungu awabariki Wakenya, abariki nchi yetu na aendelee kutulinda wakati huu mgumu.

Ahsanteni sana.

  

Latest posts

NBK’s Majikonnect programme gets Ksh 1.2B boost from WaterEquity

Ronald Owili

MSEA five years investments in small businesses top Ksh 2.8B

Ronald Owili

Evergrande gets $818m as football stadium land deal cancelled

Ronald Owili

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More