Baadhi ya wanasiasa wa chama cha Wiper katika Kaunti ya Mombasa wamemtaka mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir kumuomba msamaha kinara wao Kalonzo Musyoka kufuatia hatua ya kumataka aje amenyane naye katika kinyang’anyiro cha Ugavana wa Mombasa.
Akizungumza siku mbili zilizopita Abdulswamad alimtaka Kalonzo kufanya hivyo hata baada ya kumtangaza aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko kamba ndiye atakayepeperusha bendera ya Wiper ili kumrithi gavana wa sasa Ali Hassan Joho.
Wakiongozwa na Mwakilishi wa Wadi ya Kipevu Faith Mwende, wanasiasa hao wanasema kwamba Abdulswamad amemkosea heshima Kalonzo kwani hadhi yake ya kisiasa ni ya juu kuliko shinikizo hilo.
Kwa mjibu wa Abdulswamad, Kalonzo alikuwa na njama fiche ya kumkandamiza Kinara wa ODM Raila Odinga na wala si kwa manufaa ya Chama cha Azimio la Umoja One Kenya jinsi ambavyo imekuwa ikitajwa.