Mbunge wa mvita Abduswamad Sharif Nassir ndiye atakayepeperusha bendera ya chama cha ODM katika kinyang’anyiro cha ugavana kaunti ya Mombasa. Haya yakiwa makubaliano ambayo yameafikiwa baada ya kikao cha majadiliano kuandaliwa huko jijini Nairobi kilichoongozwa ni kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.
Naye mwanabiashara Suleiman Shahbal ambaye alikuwa amejitokeza kugombania tiketi hiyo ya ODM ameahidi kushirikiana na Abduswamad kuhakikisha ODM inashinda kiti hicho cha ugavana kaunti ya Mombasa.
Abduswamad naye ameahidi kushirikiana na Shahbal ili kuhakikisha wanachanganya manifesto zao pamoja kama njia ya ya kutoa huduima bora kwa wananchi wa Mombasa endapo watashinda kiti hicho kwenye uchaguzi ujao.