Achanai gavana wa Kwanza Pwani

Eneo la Pwani limeandikisha historia kwa kuwa na mwanamke gavana kwenye uchaguzi wa mwaka 2022 uliokamilika.

Fatuma Achani  ni miongoni mwa Magavana saba waliochaguliwa kwa kushinda kiti hicho kwa tikiti ya UDA baada ya kupata kura elfu 59, 674 na kumshinda mgombea wa ODM Hamadi Boga aliyepata kura elfu 53,972

Achani ambaye ni wakili amekuwa naibu wa gavana wa kaunti hiyo.

Na mwenzake Susan Kahikia alimshinda gavana wa sasa  Lee Kinyanjui kwa kupata kura 440,707 kwa tikiti ya UDA huku Kinyanjui akipata kura 325,623. Aliwashinda wapinzani saba na kunyakuwa kiti hicho.

Naye Gladys Wanga wa ODM anakuwa gavana wa kwanza katika kaunti ya Homa Bay. Alimshinda gavana wa zamani wa Nairobi kwa kupata kura 244,559 dhidi ya Evans Kidero aliyepata kura 154, 182.

Also Read
Maafisa wa Polisi Waanzisha Msako Kuwakamata Wauzaji wa Pombe Haramu Pwani

Wanga amekuwa akihudumu kama mbunge wa kaunti.

Cecily Mbarire sasa ndiye gavana wa kwanza wa Embu na alishinda uchaguzi huo kupitia tikiti ya UDA kwa kupata kura 108,610 dhidi ya mpinzani wake Seneta wa zamani Lenny Kivuti wa chama cha DEP aliyepata kura 105,246.

Mbarire alikuwa mbunge wa zamani wa Runyenjes

 

Kawira Mwangaza aliwania kama mgombea huru na kuvunja rekodi kwa kupata kura 209,148 dhidi ya mpinzani wake ambaye ni seneta wa Meru Mithika Linturi aliyepata kura na kuwa gavana wa kwanza Meru aliyepata kura 183,859, na kufuatiwa na gavana anayeondoka Kiraitu Murungi aliyepata kura  110,814.

Also Read
Achani Amjibu Mwashetani

Wavinya Ndeti pia anakuwa gavana wa kwanza kusimamia kaunti ya Machakos baada ya kuwania waadhifa huo mara mbili akishindwa.  Alipata kura 226,609 na kufuatiwa na Nzioka Waita aliyekuwa mkuu wa wafanyakazi katika ikulu aliyepata kura 129, 181.

Mwaka 2007 alichaguliwa kama mbunge wa Kathiani kwa tikiti ya chama cha Uzalendo na kuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kama mbunge eneo hilo tangu Kenya kujipatia madaraka.

Also Read
Tanzania Yawekewa Vikwazo Na Marekani.

Na hatimaye Anne Waiguru alifanikiwa kuhifadhi kiti chake kwa tikiti ya chama cha UDA baada ya kupata kura 113,008 na kumshinda Wangui Puriy aliyepata kura 105,677.

Waiguru alihudumu kama waziri wa ugatuzi na mipango katika serikali ya rais rais Uhuru mwaka 2017.

Wajumbe wa kaunti hiyo pia walipiga kura ya kutokuwa na imani naye lakini akaokolewa na bunge la senate.

Waiguru alikuwa miongoni mwa magavana watatu waliofanikiwa kuibuka washindi kwenye uchaguzi uliopita. Wengine ni Joyce Labaso wa Bomet aliyefariki na Charity Ngilu wa Kitui.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi