Naibu gavana wa kanuti ya Kwale Bi Fatuma Achani amewataka wapinzani wake kukoma kumchafulia jina katika azma yake ya kuwania ugavana wa jimbo la Kwale.
Kwenye mahojiano na runinga moja ya humu nchini Achani amewarai wapinzani wake kuuza sera zao kikamilifu badala ya kumchamfulia jina akisema kuwa hatua hio hatua hio inahujumu usawa wa kikatiba.
Achani amesisitiza haja ya viongozi kuhubiri Amani hususan msimu huu ambapo siasa zimeshika kasi akisema kuwa matamshi ya chuki na uchochezi yanarudisha nyuma Amani ya kaunti ya Kwale.
Amewaomba wakaazi wa kaunti ya Kwale kumpigia kura ifikapo Agosti 9 huku akiwa na Imani kuu kuwa ataweza kuendeleza kazi iliyoanzishwa na gavana Mvurya kwa kikamilifu.