Acheni kuwagonganisha wakenya,Ruto awaonya wanasiasa.

Naibu rais Dr. William Ruto ametoa wito kwa wanasiasa kusita kuwagonganisha waKenya kwa manufaa yao binafsi kisisitiza kuwa ghasia hazipaswi kuruhusiwa kamwe kupenyeza katika siasa za taifa hili.

Also Read
Madereva Wa Bodaboda Kaunti Ya Kilifi Wameombwa Kudumisha Heshima Kwa Polisi

Akiongea nyumbani kwake huko Karen wakati wa hafla ya maombi iliyohudhuriwa na viongozi wa kidini na kisiasa kutoka kaunti ya Narok,naibu rais alisema kuwa wakenya wanataka viongozi wenye ajenda ya maendeleo kwa taifa hili.

Also Read
Kenya Kushirikiana Na AU

Aliongeza kwamba wanaonufaika na migawanyiko,chuki na ghasia za kisiasa watapigwa na butwaa kwa vile wakenya wanataka umoja huku akiwahakikishia wakenya kwamba serikali haitaruhusu wanaoeneza siasa duni kufaulu.

Also Read
Mtoto wa kwanza wa marehemu Kajembe afariki

Naibu wa rais vile vile alisema serikali itahakikisha kwamba mfumo wa ugavi wa mapato unawanufaisha wakenya wote kwani ilichaguliwa kuwahudumia wakenya wote bila kuwabagua.

  

Latest posts

Rais Uhuru afanya mabadiliko kwenye vikosi vya ulinzi vya Kenya KDF

Joshua Chome

Sijaagiza kukamatwa kwa majaji asisitiza Noordin Haji

Joshua Chome

Jaji mkuu awahakikishia majaji uhuru wa utekelezaji wa majukumu yao

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi