Agizo La Waziri Kagwe La Kuwataka Wakenya Wachanjwe Dhidi Ya Korona Laungwa Mkono

Kuli ya hapo awali ya waziri wa afya yakutoa makataa ya hadi Disemba 21 kuwa kila mkenya awe amepokea chanjo dhidi ya korona la sivyo wanyinyimwe huduma mhimu za serikali na usafiri wa umma inaendelea kuungwa mkono na viongozi mbali mbali.

Akiongea na meza yetu ya habari afisa mkuu mtendaji katika idara ya ujenzi na barabara katika kaunti ya Kilifi Kenneth Charo almaarufu Tungule amesema ni jukumu la kila mkenya kuhakikisha anajikinga kutokana na ugonjwa huo huku akiunga mkono agizo la waziri wa afya Mutahi Kagwe la kuwataka wakenya wachanjwe.

Wakati huo huo Tungule ameihimiza serikali kuhakikisha inasambaza chanjo hizo katika sehemu za mashinani ili iweze kuwafikia wakenya wengi ambao wangependa kuchanjwa dhidi ya korona.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi