Aisha Jumwa Kashinda na Mung’aro

 

Gideon Mungaro Maitha ndiye gavana mteule wa kaunti ya Kilifi. Na sasa anamrithi gavana anayeondoka Amason Jeffa Kingi. Mungaro  aliwashinda wapinzani wake sita kwa kupata kura 143, 772 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Aisha Jumwa mara dufu zaidi aliyepata kura elefu 65,893. George Kithi aliyewania kiti hicho kwa tikiti ya chama cha PAA alimufuatia karibu Bi. Jumwa na kupata kura elfu 64,326.

Naye Seneta Stewart Madzayo amehifadhi kiti hicho kwa mara ya tatu mfulilizo kwa kupata kura 144,740.

Gertrude Mbeyu amehifadhi kiti chake kwa mara ya pili na kuwashinda wapinzani wake watano kwa kupata kura 111,039 .

Also Read
Lalama Za Wakaazi Likoni Kuhusu Miundomsingi Duni Ya Mitaro Ya Maji Taka

Kati ya viti saba vya ubunge chama cha ODM kilinyakuwa viti vinne vya ubunge huku PAA kikipata viti mbili. Owen Baya ndiye mbugne wa UDA wa Kilifi Kaskazini aliyezoa kura elfu 27,558 .

Mbunge wa sasa wa Kaloleni Paul Katana na mbunge mwenzake Ken Chonga wa Kilifi Kusini  walihifadhi  viti vyao kwa tikiti ya ODM kwa kupata kura 16,969 na 24,300.

Wanasiasa wapya waliofanikiwa kupenya siasani  ni mbunge mteule Amina Mnyazi aliyewania kiti hicho kwa tikiti ya chama cha ODM na kuwabwaga wapinzani wanueme saba. Na sasa atakuwa anamrithi mbunge anayeondoka Aisha Jumwa. Wengine ni mbunge mteule  wa Rabai Antony Kenga aliyeshinda kwa tikiti ya chama cha PAA na mwenzake wa Magarini Harriosn Kombe aliyeshinda kiti hicho kwa tikiti ya ODM. Kati ya viti vya wadi 35, muungano wa AZIMIO ulizoa viti 17 huku muungano wa Kenya Kwanza ukipata viti 13 na tano zikichukuliwa na wagombea huru.

Also Read
Kijana Afariki Kilifi Baada Yakupigwa Na Umeme

Na kutokana na haya, wadadisi wa maswala ya kisiasa wanasema kwamba bado mgombea wa Azimio Raila Odinga na chama cha ODM kina ushawaishi katika kaunti ya hii ya Kilifi. Hata hivyo wakosoaji wengine wanahoji kwamba chama cha PAA bado ni kichanga mno kukilinganisha na chama cha ODM. Wanaelezea kwamba ingekuwa vigumu kwa gavana Kingi kuzolea kiongozi wa Kenya Kwanza kura hasa ikizingatiwa kwamba kulikuwa na wagombea wa  chama cha PAA na UDA . Kati ya wapiga kura 580,000 ni wapiga kura 289, 342 waliojitokeza kupiga kura.

Also Read
Wahudumu wa afya ya njanjani wadi marupurupu Kilifi

 

 

 

 

 

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi