Msaani Ali Kiba amezindua Rasmi Jina la Cover image ya Album yake itakayofahamika kama Only one King.
Album hii itakuwa na jumla ya nyimbo 16 huku Kiba akiweka wazi kuwa tayari amechia nyimbo nne ambazo zinapatikana kwenye Album hiyo ambazo ni Salute, Jealous Ndombolo na Ifidele.
Kuhusu uamuzi wa kulipa Jina la ONLY ONE KING, Kiba amesema kuwa ni jina ambalo lipendekezwa na Shabiki wake na aliamua kulitumia kwa kuwa yeye ndiye mfalme wa muziki wa Bongo Fleva.
Album hii ni ya tatu kwa msaani Ali Kiba ambaye aliachia Album ya kwanza mwaka 2007ilofahamika kama Cindarela na Ali K 4 Real iliotoka mwaka wa 2009.
