Eneo la Pwani litasheheni mirindimo ya kisiasa juma hili kufuatia Ziara ya kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga inayoanza hapo kesho Jumamosi tarehe tarehe 19 na kumalizika Jumanne tarehe 22.
Kingozi huyo wa Muungano wa Azimio la Umoja ataanzia Ziara yake Kaunti ya Kilifi Jumamosi kisha kuzuru kaunti ya Mombasa siku ya Jumapili.
Jumatatu atakuwa Kwale na hatimaye kukamilisha Ziara yake katika kaunti ya Taita Taveta Jumanne tarehe 22.
Wagombea wa viti mbali mbali wa Chama cha ODM watarajiwa kuonyeshana umaarufu wao kwenye Ziara hiyo inayofanyika kabla kura za mchujo.
Beatrice Gambo ni mgombea wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Kisauni na anaeleza kwamba wako tayari kwa ziara hiyo la Azimio ambapo mipango yote imekamilika.
Kwa mujibu wa Bi. Gambo amewahimiza viongozi wa eneo la Pwani kuja pamoja ili wajadiliane na kushirikiana kwenye harakati za kuhakikisha muungano wa Azimio la Umoja unaibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu ujao tarehe 9 Agosti mwaka huu.
Ziara ya Kinara huyo wa kundi la Azimio la Umoja inafanyika wiki mbili baada ya Kiongozi wa Chama cha UDA makamu wa Rais Dkt. William Ruto kufanya Ziara yake huko Pwani.