Mgombeaji wa urais wa muungano wa Azimio la umoja– One Kenya, Raila Odinga ameunda jopo la watu saba kusaka mgombea mwenza wake.
Wanachama wa jopo hilo ni Bishop Peter Njenga, archbishop Zacheous Okoth, Seneta Enoch Wambua, Michael Orwa, Noah Wekesa, Sheikh Mohammed Khalifa, na Beatrice Meo.
Kulingana na Junet yule ambaye atateuliwa kama mgombea mwenza lazima awe anaafikia vigezo muhimu vya katiba kama vile uadilifu, heshima kwa wananchi na awe mtu aliyejitolea kutumikia taifa.
Jopo hilo linafaa kuwapiga msasa wanaotaka kuchukuwa nafasi ya mgombea mwenza wa Raila na kisha kuwasilisha jina au majina ya waliofuzu kwa baraza kuu la muungano huo kabla ya tarehe 10 mwezi Mei.
Jopo hilo litaongozwa na Beatrice Meo kama mwenyekiti wake.
Akitangaza majina ya wanachama wa jopo hilo, katibu wa baraza la muungano wa Azimio – One Kenya, Junet Mohamed amesema kwamba Raila aliteua jopo hilo baada ya kushauriana na baraza kuu la muungano huo.