Baba Mbakaji Asakwa Magarini

Maafisa wa Polisi huko Marererni eneo bunge la Magarini Kaunti ya Kilifi bado wanaendelea na uchunguzi kuhusu kisa ambapo mwanamme mmoja katika mtaa wa Muyu wa Kae anadaiwa kumbaka bintiye mwenye umri wa miaka miwili na miezi kumi na moja.
Afisa msimamizi wa kituo cha Polisi cha Marereni James Kago amethibitisha kisa hicho nakusema kuwa Kingi Kitsao Mwarandu bado yuko mafichoni akisakwa na maafisa wa usalama baada ya kutimiza uovu huo.
Mamake msichana huyo ameshikikilia kwamba lazima mumewe achukuliwe hatua kali za kisheria.
Kazungu Ngalla ambaye ni chifu wa eneo hilo amesema tayari wameanzisha uchunguzi wa kina kuhusu kisa hicho huku akitoa wito kwa kwa familia kuwa na utulivu katika kipindi hiki huku Mzee wa Mtaa wa Muyu wa Kae Karisa Jondhe akisema kwa kipindi cha miezi mitatu amepokea zaidi ya visa kumi vya unajisi.
 

  

Latest posts

Nitawatetea Wanawake Vilivyo Asema Masito

Clavery Khonde

Nitaiboresha Idara Ya Usalama Kaunti Ya Mombasa Asema Abdullswamad Shariff Nassir

Clavery Khonde

Mpango Wa Wanawake Wazinduliwa Kwlae

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi