Balozi wa Marekani:Marekani Inasaidia Kenya Kwenye Vita Dhidi ya COVID-19

Balozi wa Marekani nchini Kenya Eric Neendler hii leo katika mahojiano ya moja kwa moja na Pwani Fm katika kipindi cha Dobe Dobeza amesema kuwa taifa la Marekani limetoa zaidi ya barakoa milioni 2 kwenye taifa la Kenya ili kusaidia wakenya kujikinga dhidi ya janga la Covid-19 ambalo limekuwa janga la ulimwengu mzima. balozi huyo pia amesema kuwa wamefikia sehemu zisizo na taasisi za afya na vile vile kusaidia katika utoajiw a huduma za kiafya.

Also Read
Mwendwa aitaka CAF kusimamia vipimo vya corona kwa Wachezaji

Balozi huyo pia amesema kuwa katika safari yake ya eneo la Bamba katika kaunti ya Kilifi ameweza kukutana na baadhi ya viongozi na makundi mbali mbali ya eneo hilo na akafanya mazungumzo nao kuhusu jinsi gani wanaweza kushughulikia swala la baa la njaa katika kaunti ya Kilifi hasa katika eneo hilo.

Also Read
Rashford kukosa pambano la AC MILAN
Also Read
Raila Odinga Atarajiwa Kukutana na Viongozi wa Mlima Kenya

Kwa kauli yake balozi huyo wa Marekani pia amesema kuwa mradi kamili wa ukulima huenda ukachukua kipindi cha miaka miwili ili kupata mazao mazuri na ambayo yanaweza kuwafaidisha wakaazi wote wa kaunti ya Kilifi na hasa wakaazi wa Bamba.

  

Latest posts

Wafanyibiashara Katika Soko La Malindi Walalamikia Uchafu na Uvundo.

Sylvester Chibero

Wakenya Wametakiwa Kuwa Waangalifu Wakati Wanapoabiri Magari Msimu Huu Washerehe.

Sylvester Chibero

Tutashamiri Kwenye Mashindano Ya Mwaka Huu Ya Tong-IL Moo Do Asema Master Mwakio

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi