Baraza la Magavana Lashirikiana na NYS Kutoa Mafunzo kwa Maafisa wa Serikali za Kaunti.

Baraza la Magavana limeshirikiana na huduma ya taifa kwa vijana NYS kutoa mafunzo kwa maafisa wa seikali za kaunti.

Chini ya mpango huo, NYS itatoa mafunzo kwa maafisa wa serikali za kaunti na wasimamizi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya masuala ya kiusalama.

Kundi la kwanza la takribani wasimamizi wa vijiji 400 na maafisa wa utekelezwaji wa kaunti kutoka kaunti ya Mandera, walifuzi jana kutoka chuo cha mafunzo cha NYS huko Naivasha, baada ya kupokea mafunzo kwa miezi miwili.

Hafla hiyo ya kufuzu, ilihudhuriwa na gavana wa Mandera Ali Roba na mwenzake wa Nakuru Lee Kinyanjui.

Gavana Roba alisema mafunzo hayo yananuiwa kuwapa uwezo vijana kutoka kaunti, kabla ya kuanza majukumu yao.

Roba alitoa changamoto kwa kaunti zingine 46 kufuata mkondo kwenye mpango huo, alioutambua kuwa wa manufaa.

Kwa upande wake gavana Lee Kinyanjui alisema mafunzo hayo ni ya umuhimu japo aliitaka huduma ya NYS kulenga vijana katika ngazi za mashinani kutoa mafunzo kwa vijana Zaidi ili kuinua kiwango cha uwezo wao.

 

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi