Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limemtaka msanii wa muziki Nay wa Mitego kusitisha kupeleka kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii wimbo wake wa ‘Mama’ kwa maelezo kuwa maudhui yake yanakinzana na kanuni za Baraza hilo.
Mwanamuziki huyo ametakiwa kurekebisha mashairi ya wimbo huo kama alivyolekezwa.Kwa mtazamo wangu nafikiri hiki kilichofanywa na BASATA nafikiri hili lingeachwa kwenye Media kwa sababu kila Media ina Music Department! Hii ni kazi ya Media -@naytrueboytz