Benjamin Mkapa wa Tanzania afariki

Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Benjamin Mkapa ameaga dunia.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Rais John Pombe Magufuli alitangaza kifo cha Rais huyo wa tatu wa Jamhuri ya Tanzania, kupitia shirika la utangazaji la Tanzania leo asubuhi.

Rais Magufuli alisema Rais mstaafu William Benjamin Mkapa alifariki kwenye hospitali moja ya Dar-es-Salaam ambako alikuwa amelazwa.

Alihimiza watu wote wa Tanzania kumuombea Mzee Mkapa, akisema habari zaidi zitatolewa baadaye.

Rais mstaafu William Benjamin Mkapa alizaliwa mwezi Novemba mwaka 1938 na ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Also Read
Je ni akina nani wamefariki Tanzania mfululizo na kwa kipindi kifupi na kwa sababu zipi?

Alihudumu kama Rais wa tatu wa Jamhuri ya watu wa Tanzania kati ya mwaka 1995-2005 kabla ya kumkabidhi hatamu Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Mkapa alifariki masaa ya alfajiri hii leo Ijumaa.

Viongozi mbali mbali wanaendelea kutuma rambi rambi zao kwa watu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kufuatia kifo cha Rais mstaafu Benjamin William Mkapa, usiku wa kuamkia leo kwenye hospitali moja Jijini Dar es Salaam.

Also Read
Who Yaitaka Tanzania Kujiandaa Kwa Chanjo Ya Corona

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kupitia kitandazi chake cha Twitter alisema wa-Kenya wataendelea kumkumbuka Rais mstaafu Mkapa kutokana na wajibu aliotekeleza wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007-2008 kwa kushirikiana na aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dr. Koffi Annan na Graca Machel ambazo ziliwezesha taifa hili kurejelea hali ya utulivu.

Raila alimtaja Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kuwa rafiki mkubwa wa watu wa Kenya, na pia mwana-halisi wa bara la Afrika, ambaye aliamini kwa dhati  katika ushirikiano  wa nchi za eneo la kusini mwa Afrika na pia kiongozi mweledi duniani, aliyeamini katika ushirikiano wa kanda na kupigania ufufuzi wa jumuiya ya nchi za Afrika MAshariki.

Also Read
Tanzania Na Serikali Ya Kaunti Ya Kwale Yaboresha Biashara Za Mipakani

Mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika (AUC) Moussa Faki Mahamat, kwa upande wake alielezea huzuni kubwa kufuatia kifo cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa huku akimtaja Mkapa kuwa kiongozi mweledi ambaye atakumbukwa kwa juhudi zake za amani katika eneo la Afrika mashariki.

  

Latest posts

Nadal Atinga Nusu Fainali Ya Michuano Ya Wimbledon

Clavery Khonde

Raheem Sterling Akubali Kujiunga Na Chelsea

Clavery Khonde

Waziri Chelagui Awahimiza Vijana Kujiunga Na Vyuo Vya Kiufundi

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi