Bodaboda Malindi zatakiwa kusitisha kazi wakati wa kafyu

Mwenyekiti wa masuala ya amani na usalama mjini Malindi kaunti ya Kilifi ustadh Athman Said, amewahimiza wahudumu wa boda boda eneo hilo kuhakikisha wanazingatia masaa ya marufuku ya kutoka nje usiku.

Also Read
Dawa Ya Septrin Yatajwa Kuwa Haba

Kulingana na Said, kwa sasa idadi kubwa ya wahudumu hao wameonekana kupuuza masharti hayo yanayolenga kupambana na janga la corona.

Mwenyekiti huyo amedai kuwa huenda wahalifu wameanza kutumia fursa hiyo na kupelekea visa vya utovu wa usalama miongono mwa wahudumu hao.

Also Read
Wanafunzi wa vyuo waililia serikali.

Hata hivyo, amewataka washikadau wa masuala ya uslama kushirikiana ili kukomesha visa vya mauaji kwa wahudumu hao ambavyo vimeanza kuchipuka tena.

Also Read
Kalonzo Afika Mbele Ya Jopo La Mahojiano Ya Kutafuta Nafasi Ya Mgombea Mwenza Kusailiwa

Ameonya kuwa yeyote atakayepatikana amejihusisha na uovu huo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

  

Latest posts

Nitaiboresha Idara Ya Usalama Kaunti Ya Mombasa Asema Abdullswamad Shariff Nassir

Clavery Khonde

Mpango Wa Wanawake Wazinduliwa Kwlae

Clavery Khonde

Waziri Magoha Aahidi Uimarishwaji Zaidi Wa Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi