Mgombea wa ugavana kupitia chama cvha ODM kaunti ya Kwale Hamad Bonga amemuweka kando Safina Kwekwe Tsungu na kumchagua mgombea mwenza wake mpya Nurein Ndao Mwatsahu akiongea na wafuasi wake huko shimbahills.
Boga anasema ilimlazimu kufanya hivyo baada ya Kwekwe kuchelewa kujiuzulu akisema alikuwa anahofia kwamba kigezo hicho kingemletea matatizo na wapinzani wake kama angewasilisha jina lake kwa tume ya IEBC.
Safina kwekwe amesema ameridhia uteuzi huo akisema bado atazidi kuunga mkono azima ya Boga kuwa gavana wa Kwale.