Bunge lajadili hotuba ya rais huku mseto wa hisia ukiibuka kutoka kwa pande mbili

Mjadala kuhusu hotuba ya uzinduzi kwa mabunge yote mawili iliyotolewa na rais William Ruto, ulianza hii leo katika bunge la kitaifa huku vyama vinavyounda muungano wa Kenya kwanza vikiipongeza hotuba hiyo.

Wabunge wa Kenya kwanza wakitoa hoja ya kuwepo kwa hazina ya watu wenye kipato cha chini, mbinu ya usimamizi wa madeni na nyumba za kodi ya bei ya chini kama masuala makuu ya kuubadilisha uchumi wa nchi hii.

Also Read
Wazazi Na Serikali Imetakiwa Kushirikiana Na Watoto Kuboresha Elimu Pwani
Also Read
Kamishna wa kaunti ya Kwale awataka wazazi kuripoti mapema visa vya unyanyasaji

Hata hivyo, wabunge wa upande wa Azimio la Umoja One Kenya waliikosoa hotuba hiyo wakisema ilikosa kusisitiza kuliunganisha taifa pamoja na mbinu za kukomesha wizi wa mali ya umma.

Kutolewa kwa hoja za kufanyiwa marekebisho kwa kanuni za bunge ili kumruhusu katibu wa baraza la mawaziri kufika mbele ya wabunge kulipokelewa vyema.

Also Read
Mbunge Wa Kisauni Ali Mbogo Apuuza Azima Ya Joho Kuwania Urais.

Mabunge yote mawili yataendelea na mjadala kuhusu hotuba hiyo hapo kesho Alhamisi. 

  

Latest posts

Mvurya Ataka Maafisa Wa Idara Na Mashirika Ya Serikali Kuhusu Maendeleo Zishirikishe Serikali Za Ugatuzi

Ruth Masita

Wanawake Wajasiriamali 450 Wanufaika Na Mafunzo Ya Kibiashara Mombasa

Ruth Masita

Mahakama yamwachilia mbunge wa Sirisia John Walukhe kwa dhamana ya shilingi milioni kumi

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi