CAK Yaweka Mipango Ya Kudhibiti Vyombo Vya Habari

Mamlaka ya mawasiliano nchini CAK imeweka kanuni za utayarishaji wa vipindi ambazo zinajumuisha sehemu kadhaa miongoni mwao ni matamshi ya chuki, mienendo ya vyombo vya habari wakati wa uchaguzi na mpango wa kuhamasisha wanahabari kuhusu kile kinachotarajiwa kutoka kwao wakati taifa linapojiandaa kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Also Read
Bien aweka wazi kuwa atafanyiwa Vasecotomy

Akizungumza hapa Mombasa wakati wa warsha ya kuhamasisha vyombo vya habari kuhusu utangazaji wa uchaguzi iliyowaleta pamoja washikadau kadhaa, meneja wa mamlaka hiyo ya mawasiliano kanda ya Pwani Joseph Kamunge amesema jumba lolote la utangazaji litakalokiuka sheria zilizoainishwa litashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Also Read
Nzai Aeleza Nia Ya Kuimarisha Maisha Ya Wajane

Kwa upande wake mshirikishi wa baraza la habari kanda ya Pwani Maureen Mudi anasema baraza hilo limepewa jukumu la kuwahamasisha wanahabari kuhusu uandishi wa habari kuhusu uchaguzi na kuzingatia maadili ya vyombo vya habari wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Also Read
Media Imechangia Mashabiki Kutoelewa Mziki Wangu Asema City Boy

Wakati huo huo Bi. Mudi ameeleza kama baraza wameweka sheria za kushughulikia wanahabari ambao wanaweza kukiuka maadili.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi