Chuo cha utalii cha Ronald Ngala katika kaunti ya Kilifi kutaanza kuwapokea wanafunzi mwezi wa saba mwaka huu.
Akiongea alipozuru chuo hicho kutathmini ujenzi wake katibu katika wizara ya usalama wa ndani ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati tekelezi ya miradi ya serikali Dkt Karanja Kibicho amesema chuo hicho kimekamilika kwa asilimia 71 na karibuni kitaanza Shughuli zake.
Kibicho amesema tayari sehemu ya malazi, baadhi ya madarasa na sehemu ya kula ziko tayari huku akisema chuo hicho kitawasajili wanafunzi 250 katika awamu ya kwanza.
Anasema mradi huo unajengwa kwa awamu na kwa sasa awamu ya kwanza inaenda kukamilika.
Aidha amewahimiza wanakandarasi wanaojenga jenga chuo hicho kuhakikisha wanakamilisha mradi huo ambao ulianza kujengwa mnamo mwaka 2012 kwa wakati.