Congo Boyz Yajiandaa

Timu ya soka ya Congo Boys kutoka mjini Mombasa ambayo inashiriki ligi ya FKF daraja la kwanza zone A humu nchini imeapa kujizatiti na kufanya vyema kwenye mechi zake za msimu mpya wakati wizara ya afya na shirikisho la soka FKF itakapotoa kibali cha kuruhusiwa michezo rasmi.

Also Read
Serikali Na Jamii Imehimizwa Kupiga Vita Ukeketaji

Mkufunzi wa kilabu hio Yusuf Ndere amedokeza kuwa kwa sasa bado hajaanza mazoezi wakisubiri hatama ya wizara ya michezo lakini amekua akiwasiliana na wachezaji wake ili kuwatayarisha kisaikolojia kabla ya kurudi dimabni.

Also Read
Rais Tshisekedi hatimae apokea chanjo

Coach Ndere amekua nguzo kubwa kwa timu hio ambayo imekua ikifanya vizuri na kabla ya michezo kusitishwa humu nchini timu hio ilikua katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ya daraja la kwanza zone A ambayo inajuimuisha timu 16.

Also Read
Wanafunzi Wa Vyuo Wanafaa Kuhamasishwa Dhidi Ya Dhulma Za Kijinsia Asema Prof. Laila

Congo Boys iko chini pia ya uangalizi wa mwenyekiti wa shirika la msalaba mwekundu kaunti ya Mombasa Mahmoud Noor ambaye wakati mwingi hutoa mawaidha kwa wachezaji na kuwahimiza kuendelea kujituma na kujiepusha na madawa ya kulevya.

  

Latest posts

Nitaiboresha Idara Ya Usalama Kaunti Ya Mombasa Asema Abdullswamad Shariff Nassir

Clavery Khonde

Mpango Wa Wanawake Wazinduliwa Kwlae

Clavery Khonde

Waziri Magoha Aahidi Uimarishwaji Zaidi Wa Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi