Davido alitumbuiza katika taramasha kali liloandaliwa Ukumbi wa 02 inchini Uingereza mnamo March 5 2022 ambapo alizidisha mda aliowekewa kwa dakika 34.
Kulingana na waandalizi wa tamasha hilo huwa kuna sheria kali ya kutamatisha sherehe pindi ifikapo saa tano usiku kwa ajili ya curfew. Endapo Ukipitiliza mda huo inakupasa kulipa faini ya £10,000 kila dakika.
Licha ya kutambua hilo Bilionae Davido aliamua kuendeleza tamasha lake ili kukamilisha tamasha vyema. Hatua iyo ilimugharimu £340,000 kwa jumla.