Jarida moja nchini Africa Kusini linalochapisha taarifa kuwahusu mastaa wanaovalia vitu feki limedai kuwa viatu alivyovalia Diamond kwenye photoshot ya matayarisho ya cover photo ya tour yake nchini marekani ni feki.
Diamond aliacha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa amevalia viatu vya Gucci ila jarida la Fake Gucci community limesema kuwa Kampuni hio kufikia sasa haijawahi tengeneza viatu kama alivyovaa diamond.
Hii sio mara ya kwanza Diamond Platinumz anamulikwa kwa kuvalia bidhaa feki na kuishia kuviringishia kwenye mitandao.
