Mkufunzi wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps anatarajiwa kwa mara ya kwanza kumuita kikosini Karim Benzema kwa Mashindano ya Euro 2020 msimu huu.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid hajawahi kuitwa kwenye tiu ya taifa na meneja Didier Deschamps tangu 2015 baada ya kuhusishwa na sakata ya ngono na mchezaji mwenzake wa zamani Mathieu Valbuena.
Ripoti ya L’Equipe inasema kwamba Deschamps sasa anafikiria uwezekano wa kumuita Benzema.
Benzema anashukiwa kumhimiza Valbuena kutoa video ya ngono ambayo alihusika.
Wachunguzi ambao walishtaki Benzema wanaamini alifikiriwa na rafiki wa utotoni kufanya kama mpatanishi na kumshawishi Valbuena kushughulika moja kwa moja na wauzaji.
Badala yake, Valbuena aliwajulisha polisi.
Wakati habari hii ilipovuja, Benzema alikosolewa na wakati huo Waziri Mkuu Manuel Valls alisema mchezaji huyo wa zamani wa Lyon hatakuwa na nafasi katika timu ya kitaifa.
Inaeleweka kuwa Benzema ataendelea na kesi kutoka Jumatano, Oktoba 20 hadi Ijumaa, Oktoba 22 mwaka huu.
Tayari alikanusha makosa yoyote na watu wengine wanne ambao wanakabiliwa n mashtaka hayo katika kesi hiyo.
Hapo awali, iliripotiwa kuwa Benzema angekabiliwa na kesi mnamo Januari.
Akijibu habari za kesi hiyo, wakili wa Benzema Sylvian Cormier alielezea uamuzi huo kama “ujinga”.
Licha ya kesi hiyo kuwa juu yake, mshambuliaji huyo mkongwe amekua na msimu mzuri wake bora na ametinga mabao 29 kwenye mashindano yote hadi sasa.