EACC Itahakikisha Walioteuliwa Wanatia Saini Mkataba Wa Kujitolea

Viongozi waliochaguliwa na walioteuliwa na vyama vya kisiasa pamoja na  maafisa wengine wa  serikali watahitajika kutia saini mkataba wa kujitolea kuzingatia maadili wanapohudumu kando na kiapo cha kawaida kwa kazi zao.

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi EACC Twalib Mbarak, kwenye taarifa, amesema kuambatana na sehemu ya 40 ya sheria ya bunge kuhusu uongozi na maadili, mpango huo wa kuwataka maafisa wa serikali kutia saini mkataba wa kanuni za maadili utawaweka katika nafasi bora kudumisha maadili, kuhifadhi imani ya umma na kujiepusha na vitendo vya ufisadi.

Mbarak amesema tume hiyo inawasiliana na ofisi ya jaji mkuu na ofisi nyingine husika pamoja na kamati andalizi za hafla ya kuwaapisha maofisa viongozi waliochaguliwa kwa nia ya kuhakikisha maofisa wapya wa serikali wanatia saini mkataba wa kuhifadhi kanuni za maadili wakati wa kuapishwa.

  

Latest posts

Watoto Wanaotelekezwa Wako Hatarini Ya Kujiunga Na Makundi Ya Kihalifu Asema Hakimu Nabwana

Clavery Khonde

Rais aahidi kukomesha aibu ya njaa nchini

Joshua Chome

Mradi Wa Unyunyiziaji Mashamba Maji TanaRiver Waimarishwa

Ruth Masita

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi