ECOWAS yaweka vikwazo Guinea

Jumuia ya Kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS imewawekea vikwazo vya safari na fedha  kikosi cha wanajeshi waliopindua serikali ya Guinea, pamoja na familia zao.

Uamuzi huo, unajiri baada ya kikao maalumu cha jumuia hiyo, kilichofanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

Also Read
Viongozi wa Afrika Magharibi kujadili mzozo wa Guinea

Vikwazo hivyo vinatarajiwa kuongeza shinikizo kwa wanajeshi hao kurejesha utawala wa Katiba.

Kadhalika umoja huo unalitaka jeshi kufanya uchaguzi ndani ya miezi sita na kusisitiza kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayeruhusiwa kugombea katika uchaguzi huo.

Also Read
‘Akaunti zote za benki za serikali zifungwe,’ lasema jeshi la Guinea

Viongozi hao hata hivyo wameeleza utayari wao wa kuiunga mkono Guinea katika mchakato huo wa mpito

Aidha wametoa wito kwa Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na washirika wao wa kimataifa kusaidia utekelezaji wa marufuku ya kusafiri na vikwazo vya fedha dhidi ya wanajeshi hao na familia zao.

Also Read
Guinea Yaonywa Kuhusu Kuenea kwa Chuki Wakati wa Kampeni

Wanataka pia kutolewa bila masharti kwa Rais aliyeondolewa mamlakani Alpha Condé.

 

  

Latest posts

Mshukiwa Mkuu Wa Mauaji Ya Mwanariadha Agnes Tirop Amekamatwa Mombasa

Clavery Khonde

Mbelle Awahimiza Vijana Kuzidisha Chachu Ya Talanta Zao

Clavery Khonde

Rais Kenyatta Amekutana Na Rais Biden Wa Marekani

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi