Familia ya Chidzuga yamuidhinisha mwanahabari Aisha Chidzuga kugombea ubunge Matuga

Familia ya aliyekuwa mwakilishi wa kwanza wa kike kaunti ya Kwale marehemu Zainab Chidzuga imemuidhinisha mwanahabari Mwanaisha Chidzuga kuwania kiti cha ubunge wa Matuga mwaka ujao.

Wakiongozwa na Salim Seif Chidzuga, familia hiyo imesema kuwa imeamua kumuunga mkono Mwanaisha baada ya kukubaliana kwa pamoja.

Also Read
Naibu Rais Dkt Ruto Awasuta Wapinzani

Kwa upande wake Mwanaisha amewataka wakaazi wa Matuga kumuunga mkono katika azma yake ya kuwania ubunge wa eneo hilo.

Also Read
Gavana Dhadho Amlaumu Mtangulizi Wake Kwa Malimbikizi Ya Madeni

Huku hayo yakijiri kakaake mwanahabari huyo Hassan Chidzuga amedai kuwa familia hiyo bado haijakubaliana kuhusu suala hilo akisema dadaake hajakuwa na muingiliano vizuri na wananchi.

Hata hivyo, Hassan amesisitiza kuwa yuko debeni japo ameahidi kumuunga mkono dadaake endapo familia itamchagua.

Also Read
Tume ya uwiano na utangamano yasisitiza haja ya kufanyika kwa uchaguzi wa amani

Ikumbukwe kwamba Marehemu bi Zainab Chidzuga alikuwa na azma ya kuwania kiti cha ubunge Matuga kabla ya kifo chake.

PICHA KWA HISANI

  

Latest posts

Vijana Wametakiwa Kutosubiri Kupewa Pesa Na Wanasiasa Ili Wajiandikishe Kama Wapiga Kura

Clavery Khonde

Wakaazi Taita Taveta Wahimizwa Kupokea Chanjo Dhidi Ya Korona

Clavery Khonde

Ken Chonga Akanusha Madai Ya Ubadhirifu Wa Fedha Za Basari

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi