Familia moja eneo la Mnarani kaunti ya Kilifi inaomba serikali ya kitaifa na ya kaunti pamoja na wahisani kuchangisha nauli ya ndege ya kusafirisha mwili wa mpendwa wao aliyefariki nchini Ujerumani.
Miriam Kavindu wa miaka 58 alifariki nchini Ujerumani tarehe 29 Novemba baada ya kuugua saratani.
Beth Nduge dadake marehemu amesema wanahitaji msaada ili kusafirisha mwili huo na kumzika shambani kwake Mnarani .
Kwa upande wake Alex Mwanza mtetezi wa haki za binadamu kaunti ya Kilifi amewaomba wakaazi wa Kilifi kutoa msaada wao ili familia hio ipate fedha hizo zakuleta mpendwa wao.