Wakaazi wa wadi ya Mariakani na kaunti nzima ya kilifi wameshauriwa kuwa na umakini zaidi wakati huu wanapojadili mabadiliko ya katiba BBI.
Akiongea na wakaazi katika ukumbi wa Mariakani Dairy gavana wa kaunti ya kilifi Amason Jefa kingi amesema kuwa wakaazi hao wanapaswa kupata nakala hizo wasome na wazielewe ndiposa waweze kufanya maamuzi
Na kuhusiasa na chama cha pwani kingi amesema kuwa kuna haja ya viongozi wa pwani kuja pamoja ili waweze kutetea haki na dhulma zinazowakumba wapwani,
Kingi aidha amewasihi viongozi wa pwani kutowashurutisha wakaazi kuiunga mkono mageuzi kwa kuwahadaa na mambo ya hustler na mikokoteni.