Gavana wa Kilifi Amason Kingi amewakosoa baadhi ya viongozi wanaoendeleza propaganda kwamba ripoti ya BBI inalenga kutoa nafasi za uongozi kwa watu binafsi.
Akizungumza mjini kilifi, Kingi amesema mapendekezo yaliyonakiwa kwenye ripoti hiyo yanalenga kuwanufaisha Wakenya wote huku pia akiwahimiza viongozi walio na ufahamu wa ripoti hiyo kuwaeleimisha watu wengine ambao hawajaisoma.
Wakati huo huo, Kingi amepongeza kipengele cha kuongezwa kwa maeneo bunge ambapo kaunti ya Kilifi itanufaika na maeneo bunge manne.
Kingi ameleezea kugadhabishwa kwake na hatua ya baadhi ya viongozi wa eneo la Pwani wanaopinga ripoti hiyo.