Green Umbrella yaanzisha zoezi la kupanda miti kaunti ya Kilifi

Shirika la Green Umrella linaendelea kuboresha mazingira kupitia upanzi wa miti katika eneo la Bore Singwaya Eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.

Kulingana na mfadhili wa mradi huo Ru HeartWell shirika hilo linalenga kuhifadhi misitu ya eneo hilo na pia kupunguza ukataji wa miti na utengenezaji wa mkaa.

Also Read
Idadi Kubwa Ya Wanafunzi Wamerudi Shuleni Taita Taveta

HeartWell pia amebainisha kuwa mradi huo unalenga kusaidia jamii kupitia ujenzi wa madarasa kwa masomo ya wanafunzi na wakazi wafaidike kupitia pesa inayotokana na wageni wanaotembelea eneo hilo kujiliwaza.

Also Read
Huduma Ya Polisi Imewataka Wakenya Kutii Sheria Msimu Huu Wa Pasaka

Kwa upande wake mshirikishi wa mradi huo  eneo hilo Alex Katana ni kwamba tayari miti takribani milioni 3.9 imepandwa na mipango ya kuongeza idadi hiyo ya miti ikiendelea.

Also Read
Bunge La Kwale Kupitisha Mswada Wakukabiliana Na Majanga

Katana anasema lengo kuu ni kuhakikisha mazingira ya eneo hilo yamebadilishwa na kuepuka kiangazi cha muda mrefu ambacho kimekuwa kikishuhudiwa eneo hilo

  

Latest posts

Gor Mahia Wapiga Kalamu Harrison na Benchi Lake La Kiufundi

Clavery Khonde

Sportpesa Yatoa Vifaa Vya Matibabu Kilifi

Clavery Khonde

Hospitali Za Kibinafsi Kukataa Huduma Za NHIF Mwezi Ujao

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi