Haki Afrika Yaeleza Uchaguzi Wa Agosti 9 Haukuzingatia Haki

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu Hussein Khalid ameeleza kuwa kumekuwa na ukiukaji wa haki za binadamu katika kipindi cha uchaguzi katika maeneo kadhaa hapa mchini.

Akizungumza alipokuwa akieleza ripoti ya utathmini wa haki za binadamu iliyofanywa na shirika hilo, Khalid ameeleza kuwa kuna visa visivyopungua saba vya watu kupoteza maisha katika maeneo ya Kakamega, Kibera, na Embakasi katika uchaguzi uliofanyika Agosti 9 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Khalid hali hii isipodhibitiwa huenda ikaleta madhara katika jamii.

Kadhalika mkurugenzi huyo wa HAKI AFRIKA kwa ushirikiano na mashirika mengine ya kutetea haki za kibinadamu wamependekeza kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC sawa na serikali kuu kuzingatia kufanyika uchaguzi mara mbili ndani ya miaka mitano hatua wanayoitaja itapunguza shughuli nyingi ambazo huwepo wakati huo.

Shirika la Haki Afrika ni miongoni mwa mashirika yaliofwatilia uchaguzi mkuu mwaka huu.

  

Latest posts

Rais aahidi kukomesha aibu ya njaa nchini

Joshua Chome

Mradi Wa Unyunyiziaji Mashamba Maji TanaRiver Waimarishwa

Ruth Masita

Gavana Achani akemea wanaoendeleza kuhubiri siasa chuki Kwale

Ibrahim Nyundo

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi