Hifadhi Ya Maiti Ya Kilifi Yafungwa.

Shughuli za kuhifadhi miili katika hifadhi ya maiti ya hosipitali kuu ya kaunti ya Kilifi zimesimamishwa kwa muda wa wiki mbili.
Kulingana na msimamizi wa hosipitali ya Kilifi Timothy Musau hifadhi hiyo imefungwa kwa sababu ya kuhamisha kwa  vifaa hadi katika hifadhi mpya ambayo imejengwa.
Wakati huo huo wafanyibiashara wa kutengeneza majeneza wanasema kuwa kufungwa kwa hifadhi hiyo kutasambaratisha biashara zao.
Wakiongozwa na Munga Shoboi wanasema shughuli hiyo huenda ikachukua zaidi ya mwezi mmoja na kutatiza wakazi ambao hawana uwezo wa kupeleka miili ya wapendwa wao katika hifadhi za kibinafsi
Huduma hizo zinatarajiwa kurejelewa tarehe  14 mwezi ujao.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi