Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC katika kaunti ya Kilifi imesema ina imani itawasajili wapiga kura wengi ikilinganishwa na awamu ya kwanza iliyokamilika mwaka jana.
Haya nikulingana na mshirikishi wa tume hiyo kaunti ya Kilifi Abdulwahid Hussein, ambaye amesema wamehamasisha watu umuhimu wakujiandikisha kama wapiga kura.
Akizungumza mjini Kilifi Hussein amesema baadhi ya changamoto za ukosefu wa chakula na ukame zilichangia pakubwa kusajiliwa kwa idadi ya chini ya wapiga kura.
Kwa upande wake askofu wa kanisa la Kiangilikana jimbo la Malindi Rueben Katite amewahimiza wakaazi kujitokeza kwa wingi ili wajisajili kama wapiga kura.
Awamu ya pili ya usajili wapiga kura itaanza rasmi wiki ijayo na kukamilika Fubruari 6.