Wito umetolewa kwa wakaazi wa mji wa Voi sawa na kaunti nzima kwa ujumla kujitokeza kuthibitisha majina na vituo vyao halisi katika sajili ya Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kabla ya kutamatika kwa zoezi hilo linaloendelea kite nchini.
Hii ni baada ya kushuhudiwa idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza katika vituo vilivyoratibiwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka kiendesha shughuli hiyo, halo iliyowalazimu maafisa husika wa Tume hiyo kuzunguka nyumba kwa nyumba kama njia mojawapo ya kuwafikia wapiga kura wengi.
Tony mativo ambaye ni mmoja wa maafisa hao, mjini Voi amewarai wananchi kuzingatia zoezi hilo Ili kujiandaa kikamilifu wakati wa shughuli mhimu ya uchaguzi mkuu mwezi wa agosti.