Wagombeaji wa nyadhfa za urais kwenye uchaguzi mkuu ujao wana hadi tarehe 16 mwezi ujao kuwasilisha majina ya wagombeaji wenza wao.
Tume ya uchaguzi na mipaka nchini hata hivyo imekariri kuwa tarehe 28 mwezi huu bado ndiyo tarehe ya mwisho kwa vyama vya kisiasa kuwasilisha majina ya wagombeaji wao wa nyadhifa za mwakilishi wadi,mwikilishi wa kike,mwakilishi wa bunge na mwakilishi wa seneti.
Kulingana na tume ya IEBC hatua hiyo itasaidia tume hiyo kuwasilisha majina hayo kwa taasisi husika kwa wakati ufaao.
Vyama viwili vikuu vya kisiasa awali vilikuwa wamewasilisha tetesi za kisheria kuhusiana na kuwasilishwa kwa majina hayo ya wagombea wenza kufikia tarehe 28 mwezi huu.
Katibu mkuu wa Azimio Raphael Tuju, kiongozi wa Chama Cha Kazi Moses Kuria pamoja na katibu wa Azimio la Umoja One Kenya Junet Mohamed walikuwa miongoni mwa viongozi waliokutana na maafisa wa tume ya uchaguzi kuhusiana na swala hilo la wagombea wenza.