Jaji mkuu awahakikishia majaji uhuru wa utekelezaji wa majukumu yao

Jaji mkuu Martha Koome amewahakikishia majaji na maafisa wa idara ya mahakama kuwa idara hiyo itakuwa huru huku akiwataka kutekeleza majukumu yao bila hofu na kuzingatia sheria.

Hakikisho hilo la Koome linajiri kufuatia kukamatwa na kuhojiwa kwa majaji Aggrey Muchelule na Said Chitembwe kufuatia madai kwamba walikuwa na mpango wa kupokea hongo ya shilingi milioni tano.

Wakati huo huo,mahakama ya kikatiba imezuia idara ya ujasusi nchini DCI, dhidi ya kuwakamata pamoja na kuwashtaki Muchelule na Chitembwe hadi kesi iliyowasilishwa na chama cha mahakimu na majaji itakapoamuliwa.

  

Latest posts

ODM Yamteua Mohammed Hamid Kama Mwenyekiti Wa Tawi la Mombasa

Ruth Masita

Wafanyabiashara wa Kanda ya Afrika Mashariki Walalamikia Kupanda kwa Bei ya Mafuta Nchini

Ruth Masita

Wanakandarasi waonywa dhidi ya kuzembea kaunti ya Kwale

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi