Mwanamume mmoja wa umri wa makamo amefungwa miaka miwili bila faini baada ya mahakama ya Voi kumpata na hatia ya kuiba ng’ombe wa ajuza mmoja wa miaka 80 kutoka eneo la Saghala viungani mwa mji wa Voi kaunti ya Taita Taveta.
Akiwa mbele ya hakimu mkaazi wa Voi Frederic Nyakundi, mahakama ilibaini kuwa jamaa huyo Benjamin Mwagha aliiba ng’ombe huyo terehe 18/5/2020 hata hivyo mahakama imeelezewa kuwa ng’ombe huyo alifariki hali iliyofanya ajuza huyo Chari Mwanyoha kububujikwa na machozi mbele ya mahakama akidai ng’ombe wake.
Machozi ya ajuza huyo mlalamishi yaliwafanya hakimu Fredrick Nyakundi, karani wa mahakama hiyo
Felix Kioko sawa na mwendesha mashtaka kuamua kumchangia mama huyo elfu 20 ili aweze kununua ng’ombe mwingine huku jamaa akihukumiwa miaka miwili bila faini.
Jamaa huyo ana siku 14 za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.