Jamii Ya Wamakonde Yawataka Wanasiasa Kutowashurutisha Kuwapigia Kura

Jamii ya Wamakonde yenye asili ya Msumbiji inayoishi kaunti ya Kwale imewataka viongozi wa kisiasa kutowashurutisha kuwapigia kura katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Mwenyekiti wa jamii hiyo Thomas Nguli amewataka viongozi hao kuiruhusu jamii hiyo kufanya uamuzi wao wenyewe bila kulazimishwa.
Akizungumza katika eneo la Shimba Hills, Nguli amesema kwamba jamii hiyo itawachagua viongozi wenye sera zinazoendana na matarajio yao.
Wakati huo huo, Nguli amewaonya viongozi hao dhidi ya kuchochea jamii hiyo hasa wakati huu wa msimu wa siasa.
Amewataka wanasiasa kuepukana na visa vya uchochezi vinavyotishia umoja wa jamii hiyo.
  

Latest posts

Gor Mahia Wapiga Kalamu Harrison na Benchi Lake La Kiufundi

Clavery Khonde

Sportpesa Yatoa Vifaa Vya Matibabu Kilifi

Clavery Khonde

Hospitali Za Kibinafsi Kukataa Huduma Za NHIF Mwezi Ujao

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi