Jamii Zilizoathirika na Uchimbaji Madini Kwale na Mombasa Watarajiwa Kufidiwa

Zaidi ya shilingi milioni 200 zimetengewa kamati ya mkataba wa maendeleo ya jamii zilizoathirika na shughuli za uchimbaji madini (CDAC) katika kaunti za Kwale na Mombasa.

Meneja msimamizi wa maswala ya jamii katika kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium Pius Kassim amesema kuwa fedha hizo ni asilimia moja ya mgao wa jamii zilizoathirika katika kaunti hizo.

Also Read
Version Mpya ya Wimbo wa Susumila 'Kiuno Wavuja'

Kulingana na Kassim, fedha hizo zimetengewa maeneo ya Msambweni, Lungalunga na Likoni yaliyoathirika na uchimbaji wa madini unaoendelezwa na kampuni hiyo.

Also Read
Wazee wahimiza kudumishwa kwa usalama Kilifi Kaskazini
Meneja msimamizi wa maswala ya jamii katika kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium Pius Kassim

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo katika eneo bunge la Msambweni Mshenga Ruga amesema kuwa shilingi milioni 15 zitatumika kwa ufadhili wa masomo ya wanafunzi wasiojiweza katika kaunti ya Kwale.

Also Read
Wanawake wahimizwa kujiunga na biashara ya boda boda kaunti ya Kwale

Ruga amedokeza kwamba fedha hizo zinawalenga wanafunzi 370 wa kidato cha kwanza waliopata alama chini ya 350 na wale wa vyuo vya kiufundi.

mwenyekiti wa kamati maswala ya jamii eneo la Msambweni katika kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium Mshenga Ruga

 

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi