Japo nimebwagwa Lakini Kilifi yabakia ngome ya ODM Asema Mwambire

Mwenyekiti wa chama cha ODM katika kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire ameshindwa kuhifadhi kiti cha eneo bunge la Ganze. Tungule Kazungu Charo wa PAA ndiye mshindi wa uchaguzi wa eneo hilo iliyepata kura 24,497. Mwambire alipata kura 11,482.

Also Read
Abduswamad Kupeperusha Bendera Ya ODM Mombasa

Kwenye taarifa iliyoweka kwenye mtandao wake wa Facebook, Mwambire asema japo hajafanikiwa lakini ameridhika  na jinsi wakaazi wa eneo hilo walivyopigia kura mgombea wa urais  wa muungano wa Azimio katika eneo hilo .

Also Read
Kamati ya kupokezana Mamlaka Yaanda kikao cha kwanza

Raila Odinga alingoza kwa wingi wa kura eneo hilo ambapo wadadisi wa maswala ya kisiasa wamehoji kwamba kiongozi wa chama cha PAA Amason Kingi alishindwa kumsaidia naibu wa rais  William Ruto mgombea wa Kenya Kwanza kuzoa kura.

Also Read
Barasa gavana mpya wa Kakamega

Mwambire alisema kwamba eneo la Kilifi Kaunti bado ni ngome ya watalii.

Mwambire alichukuwa nafasi ya Kingi kama mwenyekiti wa eneo hilo kwa tikiti ya ODM ambapo baadaye aliamua kijiunga na chama cha PAA.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi